Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli

Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli

Habari

Naibu Waziri Nishati aipongeza PURA kushiriki SabasabaNa JANETH MESOMAPYA

Leo Julai 6, 2021 Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati Stephen Byabato ametembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba.

Naibu Waziri Byabato ameipongeza PURA kwa kushiriki maonesho hayo na kueleza kuwa ni fursa adhimu kwa Mamlaka hiyo kuongeza uelewa kwa Watanzania pamoja na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya shughuli za mkondo wa juu wa petroli.

Vivyo hiyo ameipongeza kwa kazi nzuri ya usimamizi wa shughuli hizo za mkondo wa juu wa petroli nchini. Kwenye maonesho haya, PURA inapatikana banda namba 127 kwenye jengo la Karume.

Kwenye banda hilo wataalamu wa PURA wanatoa uelewa wa masuala mbalimbali ikiwemo shughuli za utafiti wa mafuta zinazoendelea nchini, hali za leseni za utafutaji, fursa zinazopatikana kwenye shughuli za mkondo wa juu wa petroli na mengine mengi.